Asali ni kimiminika chenye ladha tamu ya sukari, chenye
kunata na rangi ya manjano. Asali kama chakula na
dawa ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu.
Kwa mfano yapata miaka 4,000 iliyopita madaktari wa
tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali
kutibu magonjwa mbalimbali kama vile vidonda vya
tumbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi
na yale ya tumbo.
Faida za asali kiafya
1. Asali hutumika kama chakula hivyo huongeza nguvu
mwilini.
2. Ni kiongezeo katika vyakula kama mkate, karanga na
nafaka nyingine.
3. Hutibu vidonda mbalimbali (kama vidonda vya
kuungua na moto, mikwaruzo kwenye ngozi n.k)
4. Kwa kunywa mchanganyiko wa asali, siki na maji
katika vipimo sawa ni tiba kwani huaminika kuua
vijidudu visababishavyo magonjwa.
5. Hufanya ngozi yako kuwa nyororo na katika hali
nzuri isiyo ya ukavu wakati wote. Paka asali kwenye
ngozi na acha kwa dakika 30 kisha jisafishe. Fanya
hivyo mara kwa mara na utaona mabadiliko katika
ngozi yako.
6. Asali huboresha na kuweka nywele katika hali nzuri
wakati wote (natural hair conditioner). Changanya
kijiko kimoja cha asali na shampoo kisha tia
mchanganyiko huo kwenye nywele zako kwa dakika 20,
osha na kausha nywele zako vizuri.
7. Huondoa chunusi na kuboresha ngozi yako. Paka
asali sehemu yenye chunusi kwa dakika 30 kisha osha
ngozi yako kwa maji ya vuguvugu. Fanya hivyo kwa
siku kadhaa utaona mabadiliko.
Matumizi ya asali katika matibabu
Sehemu nyingi duniani watu wanatumia asali kutibu
magonjwa mbalimbali. Licha ya kuwa asali huongeza
kinga ya mwili, sayansi ya tiba imebaini asali bora ina
wingi wa sukari (76g/ml), tindikali (acidity, Ph =
3.6-4.2) na baadhi ya kemikali ambazo zinatokana na
viumbe hai (organic compounds) vyote kwa pamoja ni
sababu za asali kuwa ni dawa.
Virutubisho vya kiafya katika asali
Asali ni chanzo cha sukari hivyo mwili
hupata nguvu na nishati.
Asali inamchanganyiko wa virutubisho na
kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya
vitu hivyo ni sukari, vitamini, amino acids
(vitu vinavyotengeneza protini),
vimeng'enyo (enzymes)
Hayo ni machache kuhusu asali na matumizi yake kwa leo
Namba yetu ni 0622925000
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni