Alhamisi, 8 Desemba 2016

FAIDA 21 ZA ASALI MBICHI NA MDALASINI, NAMBA 5 NI MUHIMU KWA WANANDOA




Asali ni chakula muhimu sana kinachousaidia mwili katika kupambana na magonjwa mbalimbali pamoja na matatizo mengine yatokanayo na uzee.

Tafiti za wataalamu mbalimbali wa madawa lishe na vifaa tiba duniani zimedhihirisha kwamba uwezo wa asali katika kutibu huongezeka maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

1. Asali ikichanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

2. Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

3. Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

4. Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

5. Asali na mdalasini huaminika pia kuamsha hamu ya tendo la ndoa endapo itatumiwa kwa kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Hii inaokoa ndoa nyingi sana

6. Asali na mdalasini husaidia katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji.

7. Asali na mdalasini husaidia kupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

8. Ulaji wa asali pamoja na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi.

9. Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo pamoja na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

10. Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku ni muhimu pia kiafya kwani hupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu.

11. Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yanaweza kutoweka kwa kutumia mara kwa mara asali iliyochanganywa na mdalasini.

12.Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini husaidia kuimarika na kuongezeka kwa kinga ya mwili kutokana na asali kuwa na hazina kubwa ya virutubisho na madini.

13. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia.

14. Unywaji wa kila siku wa kikombe baridi cha chai iliyowekewa asali na mdalasini huimarisha afya bora na madhubuti kwa mtumiaji.

15. Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi. Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee.

16. Asali husaidia kuirudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu kama dondola na washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

17. Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni zilizofanyika nchini Australia na Japani asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani kwa kutumia kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi.

18. Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu. Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi na kisha kunywa tena alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka.

19. Asali ina uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

20. Kusukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis) kutokana na uwezo wa asali kuua bakteria.

21. Matumizi ya kila siku ya asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni.

Kwa mahitaji ya asali mbichi ambayo haijachakachuliwa tafadhali wasiliana nasi kwa 0622925000, watu wa Shinyanga mtaletewa mlipo lakini mikoani mtatumiwa

HIZI HAPA FAIDA ZA ASALI KIAFYA



Asali ni kimiminika chenye ladha tamu ya sukari, chenye
kunata na rangi ya manjano. Asali kama chakula na
dawa ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu.

Kwa mfano yapata miaka 4,000 iliyopita madaktari wa
tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali
kutibu magonjwa mbalimbali kama vile vidonda vya
tumbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi
na yale ya tumbo.

Faida za asali kiafya

1. Asali hutumika kama chakula hivyo huongeza nguvu
mwilini.

2. Ni kiongezeo katika vyakula kama mkate, karanga na
nafaka nyingine.

3. Hutibu vidonda mbalimbali (kama vidonda vya
kuungua na moto, mikwaruzo kwenye ngozi n.k)

4. Kwa kunywa mchanganyiko wa asali, siki na maji
katika vipimo sawa ni tiba kwani huaminika kuua
vijidudu visababishavyo magonjwa.

5. Hufanya ngozi yako kuwa nyororo na katika hali
nzuri isiyo ya ukavu wakati wote. Paka asali kwenye
ngozi na acha kwa dakika 30 kisha jisafishe. Fanya
hivyo mara kwa mara na utaona mabadiliko katika
ngozi yako.

6. Asali huboresha na kuweka nywele katika hali nzuri
wakati wote (natural hair conditioner). Changanya
kijiko kimoja cha asali na shampoo kisha tia
mchanganyiko huo kwenye nywele zako kwa dakika 20,
osha na kausha nywele zako vizuri.

7. Huondoa chunusi na kuboresha ngozi yako. Paka
asali sehemu yenye chunusi kwa dakika 30 kisha osha
ngozi yako kwa maji ya vuguvugu. Fanya hivyo kwa
siku kadhaa utaona mabadiliko.

Matumizi ya asali katika matibabu
Sehemu nyingi duniani watu wanatumia asali kutibu
magonjwa mbalimbali. Licha ya kuwa asali huongeza
kinga ya mwili, sayansi ya tiba imebaini asali bora ina
wingi wa sukari (76g/ml), tindikali (acidity, Ph =
3.6-4.2) na baadhi ya kemikali ambazo zinatokana na
viumbe hai (organic compounds) vyote kwa pamoja ni
sababu za asali kuwa ni dawa.

Virutubisho vya kiafya katika asali
Asali ni chanzo cha sukari hivyo mwili
hupata nguvu na nishati.
Asali inamchanganyiko wa virutubisho na
kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya
vitu hivyo ni sukari, vitamini, amino acids
(vitu vinavyotengeneza protini),
vimeng'enyo (enzymes)
Hayo ni machache kuhusu asali na matumizi yake kwa leo

Namba yetu ni 0622925000

ASALI NA MAJI YA UVUGUVUGU



FAIDA ZA ASALI
Anza Siku na maji ya vuguvugu yenye mchanganyiko wa ASALI mbichi ... Tangawizi na limao...kunywa Kabla ya kula kitu chochote tumbo likiwa wazi/tupu
Faida za kuanza siku hiv zipo nyingi sana hizi ni baadhi
1:husaidia kuyeyusha mafuta mwilini hivyo husaidia kupunguza uzito
2:Ni kinga ya U. T. I Kwan mchanganyiko huu husafisha kibofu cha mkojo
3:Husaidia kuupa mwili nguvu..
4:Huchochea mmengenyo wa chakula

Njia mojawapo ya kujua asali uliyonayo kama ni asili au imechanganywa kitu
Chukua karatasi miminia asali karatasi likiloa upande wa pili jua asali yako si asilia yaani imechanganywa na maji na Sukari...ila karatasi lisipoloa jipigie makofu asali yako ni asilia

Kwa mahitaji ya asali asilia ambayo haijachanganywa chochote nipigie 0622925000 kama upo Shinyanga nitakuletea popote ulipo, mikoa mingine tunakutumia

Plz nisaidie kushare